The United States Government Celebrates Five Years of Improving the Quality of HIV, TB, and Family Planning Health Services through USAID Boresha Afya North-Central and Southern Zone Activities

English (Toleo la Kiswahili hapa chini)

DODOMA, Tanzania (November 11, 2021) — Today, representatives from the United States government and the government of Tanzania celebrated the achievements of the U.S. Agency for International Development’s (USAID) Boresha Afya (“Improve  Health”) North-Central and Southern Zone activities. Through strong collaboration and enduring partnership with the government of Tanzania, the $222 million, five-year Boresha Afya activities improved health outcomes for millions of Tanzanians in 12 regions across the country.

HIV, malaria, and tuberculosis (TB) are among the leading causes of illness, disability, and death in Tanzania. The lack of access to maternal/child health and family planning services for Tanzanian citizens, especially for women and adolescents, also contributes to poor health. Too many Tanzanians are unable to access high-quality, inclusive health services, with limited coordination between facilities and communities resulting in inadequate support for patients.

Over the last five years, the Boresha Afya activities employed dynamic and innovative solutions to address these challenges. The activities’ primary objectives were to increase the availability of- and improve access to- quality health services at the community level. To achieve its objectives, the activities combined HIV services with sexual/reproductive health, TB, and family planning services, and coordinated between health service providers, and communities.

As a result of the Boresha Afya activities, over 8.3 million Tanzanians received HIV testing services of which nearly 340 thousand learned their HIV-positive status. All HIV-positive patients were enrolled on life-saving antiretroviral treatment. Furthermore, Boresha Afya reached over 10 million clients through the provision of family planning outreach services.

Speaking at the event, USAID Mission Director V. Kate Somvongsiri addressed the guest of honor, Minister of the President’s Office for Regional Administration and Local Government, Ummy Mwalimu. “Honorable Minister, we hope the achievements highlighted in this meeting will encourage your ministry to maintain an enabling environment that will continue to support an integrated approach to health services delivery for all Tanzanians so that these achievements can be sustained.”

For more information about this press release, please contact the U.S. Embassy Tanzania Press Office at DPO@state.gov.

Serikali ya Marekani inaadhimisha miaka mitano ya kuboresha huduma za afya ya VVU/ UKIMWI, KIFUA KIKUUna uzazi wa mpango kupitia miradi ya USAID Boresha Afya Kanda ya Kaskazini na Kusini.

DODOMA, Tanzania (Novemba 11, 2021) — Leo, wawakilishi kutoka serikali ya Marekani na serikali ya Tanzania wamesherehekea mafanikio ya miradi ya Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Boresha Afya Kanda ya Kaskazini-Kati na Kusini. Kupitia ushirikiano mkubwa na wa kudumu na serikali ya Tanzania, miradi ya Boresha afya ya dola za Marekani  milioni 222, iliboresha matokeo chanya ya afya kwa mamilioni ya Watanzania katika mikoa 12 nchini kote.

VVU, malaria, na kifua kikuu ni miongoni mwa sababu kuu za magonjwa, ulemavu na vifo nchini Tanzania. Kukosekana kwa huduma za afya ya mama na mtoto na uzazi wa mpango kwa raia wa Tanzania hasa kwa wanawake na vijana pia kunachangia afya duni. Watanzania wengi hawawezi kupata huduma bora za afya kutokana na  uratibu duni  kati ya vituo vya afya na jamii.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, miradi ya Boresha Afya ilitumia njia  madhubuti na ubunifu wa hali ya juu  kushughulikia changamoto hizi. Malengo makuu ya miradi hiyo yalikuwa ni kuongeza upatikanaji- na kuboresha huduma bora za afya katika ngazi ya jamii. Ili kufikia malengo yake, miradi ilijumuisha huduma za VVU/UKIMWI, afya ya uzazi,kifua kikuu na uzazi wa mpango.

Kama matokeo ya miradi ya Boresha Afya, zaidi ya Watanzania milioni nane nukta tatu  walipata huduma za kupima VVU ambapo karibu  watu  laki tatu na arobaini  waligundulika wanaishi na  VVU. Wote walianzishiwa matibabu  ya kuokoa maisha kwa kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU. Zaidi ya hayo, Boresha Afya iliwafikia zaidi ya wanufaika milioni 10 kupitia utoaji wa huduma za uzazi wa mpango

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkazi wa USAID V. Kate Somvongsiri akizungumza na mgeni rasmi, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu. “Mheshimiwa Waziri, tunatarajia mafanikio yaliyoainishwa katika mkutano huu yatahimiza wizara yako kuweka mazingira wezeshi yatakayoendelea kusaidia mfumo shirikishi wa utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania wote ili mafanikio haya yaweze kuwa endelevu.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kupitia DPO@state.gov